Duration 2:46

*KATIBU MKUU WA CCM NDG. DANIEL CHONGOLO AWATAKA WABUNGE WA UWT KUSIMAMIA KWA UTOAJI WA Fedha

77 watched
0
3
Published 26 Jun 2021

*KATIBU MKUU WA CCM NDG. DANIEL CHONGOLO AWATAKA WABUNGE WA UWT KUSIMAMIA KWA UTOAJI WA FEDHA 4% ZA WANAWAKE* Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Daniel Chongolo amewataka wabunge wananaotokana na Jumuiya ya wanawake Tanzania (UWT) kusimamia kwa karibu utoleawaji wa fedha za mikopo ya wanawake katika Halmashauri zote nchini. Ameyasema hayo alipokuwa akifungua kikao cha Kawaida Cha Baraza Mkuu la UWT kilichofanyika katika ukumbi wa NEC Makao Makuu ya Chama Dodoma leo tarehe 26 Juni, 2021. "Wabunge wa UWT wote, wakae waandike taarifa kwenye kila maeneo yao wanapotoka au mkoa anapotoka kuhusu asilimia nne (4%) ya fedha za Halmashauri walivyozisimamia na zilivyoleta tija katika eneo hilo kwa wanawake, lakini na namna walivyowasilisha kwenye vikao vyao ngazi ya wilaya na mikoa ili kuleta muunganiko na usimamizi wa karibu wa fedha hizi." Aidha katika pamoja na mambo mengine, Katibu Mkuu ametoa msisitizo kwa viongozi wote wa UWT kuweka mkazo katika kukutana na kufanya vikao kuanzia ngazi za matawi walipo wanachama na wananchi, ukilinganisha na ngazi zingine ambapo vikao uhusisha viongozi pekee. Imetolewa na; Said Said Nguya Afisa Habari Ofisi ya Katibu Mkuu CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)

Category

Show more

Comments - 0