Duration 12:59

Jengo jipya la abiria MWANZA AIRPORT liko kitaalam sana- Mongella

6 857 watched
0
33
Published 28 Oct 2019

Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali amekagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la abiria katika uwanja wa ndege wa Mwanza na kuridhishwa na kasi ya ujenzi wa jengo hilo litakalogharimu Bilioni 12 hadi kukamilika Aprili, 2020. Ujenzi huo katika hatua ya awali ya msingi umefikia asilimia 60 ambapo kazi inafanyika usiku na mchana ili kufikia malengo ya kukamilika ndani ya miezi sita badala ya miezi 12 kama ilivyopangwa hapo awali. Hatua ya ujenzi wa jengo hilo jipya na la kisasa ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Rais Dkt. John Magufuli alilolitoa Julai 15, 2019 wakazi akizindua miradi ya afya katika Hospitali ya Rufaa Bugando ambapo Halmashauri za Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela zinachangia shilingi bilioni nne kwenye ujenzi huo. Mradi huo unasimamiwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza kwa kushirikiana na Wataalam kutoka Halmashauri za Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela kupitia mfumo wa "Force Account".

Category

Show more

Comments - 10